Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , imesema Watendaji na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa inadaiwa chanjo cha migogoro ya Ardhi Mkoani Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati wa kuzindua Masta plani ya Mkoa katika ukumbi wa Arnatogluo Wilayani Ilala.
“Mkoani Dar es Salaam migogoro ya Ardhi imekithiri na migogoro mingi inadaiwa kuchangiwa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Watendaji Kata wa Wilaya ya Kinondoni wanatoa vibali kwa shilingi 700,000/=alisema Lukuvi
Waziri Lukuvi alisema baadhi ya Watendaji wamekuwa sio waminifu kwa kutumia madaraka yao vibaya katika huuzaji Ardhi kiholela .
Akizungumzia matapeli wa Ardhi Dar es Salaam alisema matapeli ya Ardhi wanajulikana kwa majina na baadhi yao amewapiga marufuku W izarani kufika kwa sababu walikuwa wakiwatapeli wananchi.
Waziri Lukuvi akizungumzia mpango wa Masta Plani alisema mpango wa masta plani hauwezi kuathiri mtu anayeitaji kubadili eneo anatumia fursa ananunua kwa kuwalipa
Lukuvi alipongeza kila Halmashauri kwa uundwaji wa mpango huo wa masta plani kabambe ya awamu ya pili mwaka 1968 alisema mpango wa masta plani umeandaliwa mwaka 2016 unalenga kuboresha Jiji la Dar es Salaam kwa kujenga magorofa ya kisasa .
Aidha Lukuvi alisema kuwa masta plani hiyo ya Dar Es Salaam itakuwa na sehemu za vitovu vya biashara 23 vitakavyovutia Jiji hilo zikiwemo Mwenge ,Ubungo.
Ameagiza kuendeleza Makazi yasio rasmi na katika makutano ya Barabara yote kujenga majengo ya kisasa ili mji huo uweze kuvutia.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari