November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Ardhi kufanya tathmini hali ya maafa Hanang

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Eng. Anthony Sanga amewasili katika Kijiji cha Gendabi Wilaya ya Hanang pamoja na wataalamu ya Wizara kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya maafa yaliyoasababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Nchini kote.

Aidha Eng. Sanga ameunda timu ya Wataalamu mbalimbali itakayofanya kazi ya tathmini ya maafa hayo kufuatia maporomoko ya magogo,mawe na matope yaliyosababishwa na mvua, zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Pamoja na mambo mengine timu hiyo ya wataalamu itafanya tathimini ya kiwango cha uharibifu wa mali,makazi na Shughuli za wananchi.

Hatua hii ya Katibu Mkuu Sanga kutekeleza maagizo ya haya Waziri Mkuu ya kuitaka serikali kufanya tathmini ya hali maafa ili wananchi waliokumbwa na maafa waweze kutokana na madhara yaliyosababishwa mafuriko hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga pamoja na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha wakiwa na Mkuu wa Operation ya uokoaji kutoka Jeshi la Zimamoto Kamishna Mbaraka Semwanza ambaye pia ni Mkuu wa operation ya maokozi wakikagua eneo la Kijiji cha Gendabi lililoathiriwa na mvua kwa lengo la kufanya uhakiki wa hali ya maafa.