December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Ardhi kidedea mashindano ya SHIWIMI

Na mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dodoma

Timu ya Mpira wa Pete ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mapema leo imekabidahi kombe la mshindi wa pili upande wa mpira wa pete baada ya kuiwakilisha vyema Wizara hiyo katika Mshindano ya SHIMIWI yaliyofika tamati jana Mkoani Iringa.

Akiongea mara baada ya kukabidhiwa Kombe hilo naodha wa kikosi hicho Bi. Scolastica Nyendo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bi. Lucy Kabyemera amewataka wanamichezo hao kujipanga kwa ajili ya mataji makubwa wakati Wizara yake itakapojipanga tena mwakani.

Naibu Katibu Mkuu Kabyemera ameipongeza timu yake hiyo kwa kuibuka mshindi wa pili na kuongeza kuwa imeiletea sifa kubwa Wizara yake na kuongezea kuwa ushindi huo ni ushindi wetu wote kama Wizara ya Ardhi Nyumba na Mawendeleo ya Makazi.

‘’Nawapongeza wote kwa kujitoa kwa moyo kwa ajili ya Wizara yetu lakini zaidi niwapongeze timu ya mpira wa pete na niseme mwisho wa mashindano ni mwanzo wa maandalizi ya mashindano mengine na mwaka hujao mtaleta makombe mengi zaidi.

Wakato huo naodha wa timu hiyo Bi.Scolastica Kaguta Nyendo ameisifu timu yake kwa kucheza na nidhamu kubwa ambayo imefanikisha kupata kombe la mshindi wa pili akiitaja nidhamu kubwa kuwa siri ya mafanikio hayo.

Bi. Nyendo ametoa shukrani zake kwa viongozi wa Wizara ya Ardhi kwa kuwatembelea mara kwa mara kitendo ambacho kimeendelea kuwapa moyo na hali ya kufanya vizuri katika mashinda hayo.

Mashindano ya Michezo ya SHIMIWI ufanyika kila la mwaka kwa lengo la kujiweka sawa kiafya lakini pia kuwajengea utimamu wa mwili na akili wachezaji mbalimbali wa serikali na kuwajenga kiafya kwa kuondokana na magonjwa yasiyoambikiza kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.