Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Wito umetolewa kwa waandishi wa habari,kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao pamoja na kutambua mipaka yao ya kazi.
Wito huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi Denis Ruiza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, katika mdahalo wa pili wa ulinzi na usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) kwa ufadhili wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania ( UTPC) pamoja na International Media Support (IMS).
Ruiza amesema,waandishi wa habari wanapaswa watambue mipaka yao ya kazi na kuheshimu maalekezo ya Jeshi la Polisi ili wasiharibu uchunguzi wa matukio ya jinai.
Pia wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na wasitoe taarifa ya Jeshi la Polisi bila uhusika wa Kamanda wa Polisi.
Amesema,suala la ulinzi na usalama wa raia na mali zao ni jukumu la kila mmoja siyo la jeshi la Polisi tu wala waandishi wa habari.
Japo jeshi la polisi limepewa majukumu maalumu ya kusimamia na kulinda amani na sheria,kukamata wahalifu,kuzuia uhalifu usitokee na kulinda mali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko anaeleza kuwa lengo la kuwakutanisha waandishi na Jeshi la Polisi ni kujenga umoja ,amani na ushirikiano katika kutekelezaji majukumu kwa waandishi wa habari.
Soko amesema, vyombo vya habari na Polisi vifanye kazi kwa ukaribu maana wote wana nia njema katika kujenga taifa hivyo kila mtu akifahamu majukumu,mipaka na kuheshimiana.
“MPC inafanya kazi ya kusimamia maadili na ueledi kwa waandishi na tunatumia kalamu zetu kuonesha , kuhabarisha na kukosoa ili kuweza kuijenga nchi na kuleta maendeleo kwa jamii,” amesema Soko.
Naye Mkaguzi Msaidizi wa Polisi,Mkuu wa Dawati la Habari Polisi Mkoa wa Mwanza Oscar Msuya, amesema waandishi wa habari wanapaswa kuheshimu taaluma yao,watii sheria bila shuruti na wafuate maelekezo yanayotolewa na Polisi wawapo katika shughuli mbalimbali kama vile maandamano na uchaguzi.
Oscar amesema,jamii inamaluzana kienyeji juu ya vitendo vya ukatili vinavyokuwa vinafanyika ndani ya jamii,hivyo amewaomba waandishi kufanya kazi na Dawati la Jinsia na watoto ili kumaliza changamoto hiyo.
Hata hivyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi,Dawati la Jinsia na Watoto Nyamagana Fortunata Mwinuka,amesema,Polisi na waandishi wa habari wajenge mahusiano pia kupitia michezo huku waandishi wa habari wawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa jamii katika kuzuia matukio ya ukatili na wasichoke kuibua vitendo vya ukatili katika jamii.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi