December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

WiLDAF waipa tano serikali kurudisha shule mabinti wanaopata mimba wakiwa shuleni.

Na David John timesmajira online

SHIRIKA la wanawake katika sheria na Maendeleo Afrika WilDAF chini ya mratibu wa kampeni hiyo kitaifa kutoka Wildaf Anna Kulaya amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu ameipongeza Serikali kwa jitihada za dhati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha vinatokomezwa kabisa hapa nchini

Amesema kuwa ukomeshwaji huo unawezesha wanawake na mabiti kushiriki kwenye shughuli za maendeleo nakwamba kwa mwaka huu kumeazishwa Mahakama maalum ya kushughulikia masuala ya familia ili kuongeza upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wanawake.

Anna ameyasema haya jijini Dar es salaam leo mbele ya Waziri mkuu kassim Majaliwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za uharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo amesema wanaipongeza Serikali kwa kuwaruhusu mabinti wanaopata mimba wakiwa masomoni kuendelea na shule baada ya kujifungua.

“MKUKI tunatoa wito kwa Serikali na wadau wote kuongeza jitihada za kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuharakasha kufikia lengo kubwa la kupunguza ,hivyo kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2022 kama ilivyoainishwa na MTAKUWWA ,zaidi kumaliza vitendo hivi na kufikia maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030” amesema Anna

Nakuongeza kuwa “Sisi kama wana MKUKI tunaamini kuwa muda sasa umefika kutengeneza kizazi kipya kinachothamini usawa wa kijinsia .amesisitiza

Anna amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu kuhusu ukatili wa kijinsia ni” EWE MWANANCHI KOMESHA UKATILI WA KIJINSIA SASA.” Kupitia kauli mbiu hiyo wanaiomba Serikali kutunga sheria ya kudhibiti ukatili wa kijinsia ( Gender Based Violence Violence Act) kwani ukosefu wa sheria mahususi ya makosa ya ukatili ni changamoto kubwa katika upatikanaji wa haki kwa watendewa na kuwatia hatiani watuhumiwa.

Amesema kuharakishwa kwa mabadiliko ya sheria ya ndoa juu ya mwaka 1971 ili kuokoa mabinti dhidi ya ndoa za utotoni .kuboresha muundo na kutengwa bajeti ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA.

Pia ameongeza kuwa kuna umuhimu wa kufuta sheria zote za kibaguzi mathalani sheria ya kimila ya mirathi ,tangazo la serikali Namba 436 la mwaka 1963 ambayo inanyima wanawake haki yao ya kikatiba ya kumiliki Mali kupitia urithi.

Anna akizungumzia siku 16 amesema kutakuwa na shughuli mbalimbali na midahalo ili kuleta mabadiliko katika nchi nakwamba shughuli hizo ni pamoja na maonyesho ya matumizi ya digitali ,kukuza usawa wa kijinsia na utawala bora ,kongamano la kitaifa kujadili ukatili wanaofanyiwa wanawake wenye ulemavu, msafara wa kijinsia( Caravan Route ) kuhamasisha uanzishwaji wa madawati ya kushughilikia ukatili.

Amesema kongamano kwa vionggozi wa dini kushiriki katika harakati za kukomesha ukatili wa kijinsia na tuzo kwa vinara 16 wa kupinga ukatili wa kijinsia zitatolewa.lakini pia alibainisha kwamba matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa na jeshi la polisi kati ya kipindi cha januari 2021 hadi septemba
2021 yanaonyesha kuwa watoto 6168 kati yao wasichana 5287 na wavulana 88.

Anna amefafanua kuwa wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kati ya hao watoto 3524 walibakwa ,637 walilawatiwa ,1887 walipata mimba na 130 walichomwa moto na kinachosikitisha zaidi ni kati ya visa vilivyoripotiwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni 3800 kesi zilizofanyiwa upelelezi ni 2368 na zilizotolewa hukumu 88 .

Mratibu wa kitaifa wa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo Afrika WiLDAF akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake