January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wilaya ya Ilala kugawa Jimbo la Ukonga na Kata

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde amesema Wilaya ya Ilala ipo katika mchakato wa kukagawanya jimbo la Ukonga na kata kabla uchaguzi 2025.

Mwenyekiti Sidde alisema hayo kata ya Chanika katika mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya kata hiyo ulioandaliwa na uongozi wa kata.

“Jimbo la Ukonga ni kubwa ccm wilaya ya Ilala tumepeleka mapendekezo yetu yawe majimbo mawili ya uchaguzi kabla uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 tutagawanya pamoja na kata na mitaa alisema side.

Mwenyekiti Said Sidde alisema mara baada mapendekezo yetu kurudi mchakato wa kugawa jimbo pamoja na Kata utafanyika haraka ili kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi wa eneo husika.

Katika hatua nyingine alisema Watendaji wazembe wa Serikali wanaokwamisha maendeleo kata ya Chanika na halmashauri ya Ilala kwa ujumla wachukuliwe hatua ili iwe mfano kwa wengine Katika halmashauri yetu atuwezi kufanya kazi na watendaji wanaokwamisha maendeleo ya Serikali na kumkwamisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan hasa anapoleta pesa za miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo alitoa wito akitaka apewe taarifa kuhusiana na changamoto na kero za wananchi ili ziweze kutatuliwa kwa wakati kila kiongozi kupokea kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati.

Alipongeza kata ya Chanika kwa mahusiano mazuri ya chama na Serikali kwa kudumisha upendo na umoja ambapo kwa sasa Chanika maendeleo yake yanakuja kwa kasi.

Aliwataka Chanika kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi mkuu mwaka 2025 akiwaomba waongeze wanachama wapya pamoja na kuwasajili katika kadi za kisasa za electonic ambapo alisema kadi 20,000 zipo njiani zinakuja na kadi 27,000 za kisasa za electonic tayari zimegaiwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya CHANIKA William Mwila, alisema mkutano huo ni Maalum kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 ambapo kata ya Chanika amesema watashinda mitaa yote na kushika dola.

Mwenyekiti William Mwila alisema Chanika wamejipanga vizuri chama pamoja na Jumuiya zote kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ambapo alisema kata ya Chanika itaendelea kuwa ngome ya CCM kuanzia Serikali za mitaa,Udiwani, Ubunge na kura za Rais chama cha Mapinduzi kutashinda nafasi zote .

Kata ya Chanika pia walizindua mashina matatu ya CCM Tawi la Tungini kwa ajili ya uhai wa Chama ambapo mashina yote hayo yalizinduliwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde.