Na Mwandishi wetu ,Morogoro
AMLAKA za maji na usafi wa mazingira za Moshi, Nzega na Biharamulo zimetwaa tuzo za mamlaka bora nchini, katika tathmini ya ripoti ya EWURA ya utendaji wa mamlaka za maji iliyozinduliwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso mjini Morogoro.
Aidha, mamlaka 27 zilitambuliwa kwa kuwasilisha kwa asilimia 100 tozo ya udhibiti.
Taarifa hiyo ya Tathmini imepima Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 83 zinazotoa huduma katika mikoa, wilaya na miji midogo , katika hafla iliyofanyika mjini Morogoro.
Waziri Aweso ameipongeza EWURA kwa kuandaa taarifa hiyo muhimu iliyobainisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji huduma za maji na usafi wa mazingira nchini.
Kwa mujibu wa EWURA, tathmini hiyo imeonesha mafanikio katika ongezeko la uzalishaji wa maji kwa 19.3%, wateja kufikia milioni 1.8 na mapato kuongezeka kwa 14%. Hata hivyo, changamoto kama upotevu wa maji (42.3%) na uhaba wa miundombinu ya majitaka bado zinaendelea.
Aweso amezitaka mamlaka za maji kuendelea kuboresha huduma kwa kuzingatia ubora, uwazi na uendelevu.



More Stories
Serikali yatangaza fursa za uwekezaji nishati za Dola Bil.12.9
Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum
Wanafunzi FDC waaswa kuwa mabalozi wa ulinzi wa mlaji