Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Asasi za kiraia(Azaki) inatarajia kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Azaki, Asasi chache kutoka nje ya nchi, wanazuoni,watunga sera,wananchi,viongozi pamoja na wadau wa teknolojia katika wiki ya Azaki ambayo inatarajiwa kuanza jijini Arusha October 23 mpaka October 27
Hayo yamebainishwa jijibi Arusha mapema leo na Mwenyekiti wa wiki ya Azaki Nesia Mahenge wakati akizungumza na vyombo vya habari Kuhusiana na wiki hiyo ya Azaki
Alisema kuwa ndani ya wiki hiyo ya Azaki itaweza kuwa na mambo mengi ambapo yote hayo yanalenga kuiangalia jamii hasa kwenye masuala ya Teknolojia
“kauli mbiu yetu inasema kuwa Teknolojia na jamii, hapa tunapozungumzia Teknolojia tunamaanisha kuwa tutajiangalia wapi tulipotoka wapi tulipo na wapi tunakwenda”Aliongeza
Akiongelea maendeleo ya sekta ya teknolojia alisema kuwa Azaki imefanikiwa kumpata mwakilishi wa kampuni ya APPLE kutoka nchini Marekani
“kama kauli mbiu yetu inavyosema tutamleta mwakilishi wa Apple ambaye anajulikana kwa majina ya Abubakary Ally ambapo yeye kwa uzoefu wake ataweza kutupitisha katika sekta ya Teknoloji”aliongeza
Mbali na hayo alisema kuwa ndani ya wiki hiyo ya Azaki wadau mbalimbali wa mkutano huo wataweza kupitia lakini pia kujadili mada mbalimbali ambazo nazo zitalenga kwenye jamii.
Aidha alitaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na takwimu, maadili na teknolojia, ubunifu wa teknolojia kwa maendeleo endelevu, utetezi na ushirikiano
Alimalizia kwa kuwataka wananchi na wadau wengine wa Azaki kuhakikisha kuwa wanashiriki ipasavyo katika wiki hiyo ambayo pia viongozi kama Vile balozi wa Uswisi nchini Tanzania, lakini pia Mnajisi wa Ngos kutoka Zanzibar,pamoja na Meya wa Jiji la Arusha.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM