December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Zimbabwe avutiwa na Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Mikoa na Ugatuzi kutoka nchini Zimbawe, Mheshimiwa Ezra Chadzamira ametembelea banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizochini yake na kueleza kuwa Tanzania na Zimbabwe zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo na uvuvi.

Ametembelea banda hilo tarehe 06 Julai, 2024 wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Uwanja wa Sabasaba jijini Dar es salaam.
Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu: “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”.