Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Waziri wake wa Afya Nassoro Ahmed Marzui imesema inatambua kwamba afya bora ni msingi wa maendeleo ya kijamii
na kiuchumi.
Waziri Marzui ameyasema hayo Jijini Dar es salaam mapema leo Aprili 11,2025 katika uzinduzi wa wiki ya afya Zanzibar 2025 ambayo yatarajia kufanyika Mei 4 hadi 10 Ugunja na Pemba.
Amesema wiki hiyo inahusiana moja kwa moja na vipaumbele vya Serikali vilivyobainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 pamoja na Mpango wa Mkakati wa Afya wa Zanzibar III.
“Kupitia wiki hii tunatarajia kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha malengo makuu ikiwemo kongeza Uelewa wa Afya kwa Jamii kupitia kampeni za elimu, kambi za afya, na huduma za uchunguzi wa magonjwa bure, tutahamasisha wananchi kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa”amesema
Amesema wiki hiyo imelenga kukuza utalii wa Afya na kwamba Zanzibar ina nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha utalii wa afya na wellness tourism jambo ambalo litaongeza mapato ya nchi na kutoa ajira kwa vijana nchini.
Pamoja na kuboresha ubunifu na Teknolojia katika Sekta ya Afya, Kongamano la siku saba ambalo litawapa wadau fursa ya kujadili matumizi ya telemedicine, mifumo ya kidijitali ya afya, na mbinu nyingine za kisasa katika utoaji wa huduma za afya.
Vilevile amesema kupitia wiki hiyo kutafanyika kuhamasisha ushirikiano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) ambapo watatumia jukwaa hilo kuvutia uwekezaji katika sekta ya afya, kujenga miundombinu bora ya hospitali, na kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa.
Pamoja na kuimarisha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa Afya kwani wanatambua changamoto wanazokumbana nazo wahudumu wa afya na ndiyo maana Zanzibar Afya Week 2025 itaweka mkazo kwenye afya ya akili na ustawi wa wafanyakazi wa sekta ya afya.
Waziri Mazrui ameongeza, zaidi ya hayo, kutakuwa na maonyesho ya bidhaa na huduma za afya, Upimaji wa bure wa magonjwa katika eneo la tukio Nyamanzi, Unguja, kampeni za uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa jamii kuelekea kilele cha wiki hii.
Amesema uzinduzi wa pili wa wiki ya afya Zanzibar 2025 Jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati wa kuifanya Zanzibar kuwa hub ya afya kwa wageni.
Kwa Upande Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Mngereza Miraji amesema wiki ya maadhimisho ya afya Zanzibar 2025 yatatoa fursa kwa wadau kushiriki kikamilifu.
Amesema katika wiki hiyo kutatolewa vyeti katika kilele cha maadhimisho ya Zanzibar Afya Week kwa lengo la kuenzi ushirikiano na mchango wa wadhamini wetu katika kuimarisha sekta ya afya Zanzibar.
“Tunatoa wito kwa wadau wote kuungana nasi kwa namna mbalimbali iwe kwa ufadhili wa shughuli, udhamini wa programu, au ushiriki wa moja kwa moja katika utoaji wa huduma na elimu kwa jamii. mchango wenu utakuwa ni alama ya kuthamini maendeleo ya afya Tanzania”amesema
Naye Mkurugezi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabera amesema kuwa tukio la Wiki ya Afya Zanzibar inazileta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano Pamoja katika Sekta ya Afya.
Amesema Jiji la Dar es Salaam linatambua juhudi mbalimbali zinazofanywa naserikali ya Zanzibar katika kuboresha Sekta ya Afya.

More Stories
Polisi kuchunguza madai ya mwanafunzi kutupa kichanga chooni
Sekiboko ahimiza uwekezaji Elimu ya ufundi
Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti