Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wananchi kutokuamini taarifa za upotoshaji zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu chanjo nchini.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
“Hatutakubali kuona watu wachache kwa maslahi yao wakiiweka Tanzania hatarini kwa ugonjwa wa Polio,Vyombo vya usalama wachukulieni hatua wale wote wanaosambaza taarifa za uzushi na kupotosha jamii kuhusu chanjo,chanjo hizi ni salama”Alisema
Kwa upande wa chanjo Waziri huyo amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ya utoaji wa chanjo ya matone ya Polio kwa watoto wote wenye umri wa miaka mitano inayofanyika nchi nzima ni kuongeza kinga mwili kwa watoto na hivyo kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Kirusi cha Polio kilichoripotiwa kuwepo ncho jirani ya Malawi.
Aidha, amesema kampeni hiyo itakua ni ya siku nne na itafanyika kwenye vituo vya huduma za afya pamoja na kuwafuata watoto mahali popote walipo.
Hata hivyo Waziri Ummy ameitaka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kusimamia matumizi sahii ya fedha za chanjo zilizotolewa kwenye halmashauri zote nchini.
Jumla ya Watoto 10,295,316 wanatarajiwa kufikiwa kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa awamu hii ya pili ambapo awamu ya kwanza iliyofanyika katika mikoa ya Njombe,Mbeya, Ruvuma na Songwe waliwafikia watoto 1,138,949 kati ya 983,542 waliokusudiwa.
More Stories
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa
CCM ilivyotambua mchango wa wanahabari Mkutano Mkuu Maalum