Na.WAF-Dodom
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Juni 17,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Wawakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa upande wa wanawake (UN – WOMEN) katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya afya, hususan katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto na usawa wa kijinsia katika Sekta ya Afya.
Waziri ummy ameupongeza uwakilishi huo kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya na ameahidi kuendelea kushirikiana na Umoja huo ili kufikia malengo ya kuboresha huduma za afya hasa zinazowahusu wanawake katika Sekta ya Afya.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake