Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amefungua mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kuelekea mkutano wa AGRF utakaoanza Septemba 5 hadi 8, 2023.
Mafunzo hayo ya siku 3 yalianza jijini Dar es Salaam Jana Agosti 22 hadi 24, 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Waziri Ulega alisema Ujio wa mkutano huo ni fursa adhimu kwa Taifa letu kwani kunahitajika Teknolojia za kisasa kwenye uzalishaji kwenye Mifugo, uvuvi na hata kilimo.
“Mkutano huu wa leo ni muendelezo wa mkutano uliofanywa tarehe 12 July Dodoma na 14 July katika ukumbi wa Morena na leo tena tumekuja na Warsha hii kwa waandishi wa Habari lakini pia Wahariri wa vyombo vya Habari ili tupate uelewa wa pamoja kuhusu mkutano wa AGRF dhumuni, malengo na nia yake”
“Ujio wa mkutano huu ni fursa adhimu kwa Taifa letu, tunahitaji Teknolojia za kisasa kwenye uzalishaji kwenye Mifugo, uvuvi na hata kilimo,” Alisema Waziri Ulega
Waziri Ulega alisema ili Tanzania ifanikiwe kuilisha Dunia hasa nchi za jirani ni lazima uwepo uzalishaji wa kutosha.
“Tunataka tuilishe dunia hasa majirani zetu, na ili tufanye hivyo tunahitaji kufanya uzalishaji wa kutosha”
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini