December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Simbachawene: barabara ya Makose Idodoma itakarabatiwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetenga fedha kiasi cha million 626 kukarabati na kutengeneza katika barabara ya Makose kwenda Idodoma.

“Umbali wa km 25 wa kipande cha barabara utachongwa, km 21 zitawekwa changarawe na km1 kitawekwa lami ya zege. Tayari bajeti ilishatengwa katika mwaka uliopita wa fedha wa serikali itaweka fedha nyingine kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hiyo”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George simbachwene katika mkutano wa hadhara kata ya Mlalo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Fedha ya Mwaka huu itatumika kuchomoa mawe katika eneo la barabara na itamwaga kifusi na pia kuweka zege katika maeneo mengine makorofi,alisema waziri”

Aidha amehimiza wananchi kupitia serikali za vijiji kujenga utaratibu wa kukagua na kurudishia barabara pale inaponesha imebomoka, ni lazima tutunze barabara.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime na diwani wa kata ya Mpwapwa mjini amesema Halmashauri ina mpango wa kutengeneza sheria ndogo ya kukarabati majengo yote chakavu ya shule za msingi ili kujenga mazingira bora ya kujifunzia.

“Tutatunga sheria ndogo pia ya kuhifadhi vyanzo vya maji ili wananchi wasishughulike na shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka eneo la chanzo cha maj ili uoto uliopo uendelee kubakia kama ulivyo”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi katika kata ya Malolo Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Nzugilo katika Kata Mlalo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua miundo mbinu ya elimu katika shule ya msingi Nzugilo katika Kijiji cha Nzugilo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua boma la zahanati ya Mlalo iliyopo jimbo la Kibakwe ambalo Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetenga kiasi cha million 50 kwenye bajeti kukamilisha ujenzi wake.