Na mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.
“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza alisema waziri”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe George Simbachawene katika ziara aliyoifanya Kata ya Pwaga na na Luhundwa alipotembelea na kufanya Mikutano.
“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa”
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM