Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Ahmed Djellal alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo kudumisha ushirikiano bana ya Tanzania na Algeria katika kuhakikisha ustawi wa Nchi zote mbili pamoja na raia wake.
Balozi wa Algeria alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini huku akiahidi kutoa ushirikiano katika kuimarisha mahusiano yaliyopo.
More Stories
Rehema Simfukwe atoboa siri sababu kuimba wimbo wa Chanzo
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano