Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Serikali ya Tanzania imekanusha madai ya Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kwamba imewakamata Watu watatu (Dkt. Slaa, Mdude na Wakili Mwabukusi) kwasababu ya kukosoa mkataba wa Uwekezaji wa Bandari ambapo imesema madai hayo sio ya kweli bali Watu hao wamekamatwa kwasababu za kuitisha maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa X wa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye imesema “Hakuna aliyekamatwa na hakuna ambaye atakamatwa Tanzania kwa kukosoa mkataba wa Bandari na mradi , mpango, programu au sera yoyote kuhusu mkataba huo”
“Watuhumiwa wamekamatwa kwa kutishia kufanya maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani, pia kuhamasisha Wananchi kuwashambulia Polisi, wamekamatwa ili kufikisha ujumbe mzito kwa Wakosoaji wanaofikiria kufanya makosa yoyote ya kijinai”
“Kukamatwa kwa Watu hao hakuzuii uhuru wa kutoa maoni Tanzania ila ni sehemu ya hatua za kisheria zinazolenga kuzuia maandamano yanayoweza kusababisha uasi dhidi ya Serikali iliyochaguliwa Kidemokrasia”
“Tangu imeingia madarakani March 2021 Serikali ya Rais Samia imekuza demokrasia kwa kuondoa vikwazo vya kisiasa kwa Vyama vya Siasa ikiwemo kuruhusu mikutano ya kisisasa, kuruhusu Online TV na magazeti yaliyofungiwa kufanya kazi na kuboresha uhuru wa kujieleza”
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunzi
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu