Na Mwandishi wetu, TimesMajira online
Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi LIberata Mulamula (Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022.
Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa UAE nchini, Jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula ametoa salamu za pole kwa Serikali ya UAE na kuwasihi wananchi wake kuendelea kuwa watulivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na kiongozi wao.
“Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano, umoja na undugu wetu na ndugu zetu wa UAE. Kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kimewagusa pia Watanzania kwa kuwa Tanzania na UAE zina uhusiano mzuri,” alisema Balozi Mulamula.

Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan alifariki dunia tarehe 13 Mei, 2022 akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua kwa muda.
More Stories
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
Wahariri wa vyombo vya habari nchini wapongezwa
NCHIMBI: Nia ya CCM ni kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini