November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mhagama awataka watumishi kuendelea kutekeleza majukumu kwa ubunifu

Na Mwandishi Wetu 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa Baraza la Wafanyakaziwa Ofisi hiyo,kupitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/25 kwa umakini ili kuona yale yaliyotekelezwa kwa mwaka uliopita wa fedha na kuongeza ubunifu utakaowezesha rasilimali kidogo zilizotengwa kuleta matokeo makubwa zaidi kwa mwaka ujao wa fedha.

Amesema kwa kufanya hivyo wataisaidia Ofisi hiyo  kufikia malengo na watamwezesha kila mtumishi kuwajibika ipasavyo na kwa weledi ili kupata mafanikio ya pamoja.

Mhe. Mhagama ametoa kauli hiyo leo Machi 18, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Mhagama amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuwa huru katika majadiliano hasa wakati wa agenda kuu ya kupitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti

ya mwaka 2023/24 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/25 na kwa umakini ili kuona yale yaliyotekelezwa kwa mwaka uliopita wa fedha na kuongeza ubunifu utakaowezesha rasilimali kidogo zilizotengwa kuleta matokeo makubwa zaidi kwa mwaka ujao wa fedha. 

” Kujadili bajeti ya Ofisi ni mojawapo ya majukumu ya msingi ya Baraza na yameainishwa katika mkataba unaounda Baraza hili na hii ni muhimu kwa mustakabali wa utekelezaji wa majukumu ya ofisi, naamini nyote mnafahamu namna tunavyoshiriki kwa pamoja katika maandalizi ya bajeti ya Ofusi ya Waziri Mkuu kila mwaka wa fedha ili kupata zizazokidhi mahitaji ya ofisi pamoja na utekelezaji wa majukumu tuliyopewa na Rais kupitia hati idhini iliyoanzisha ofisi hii,” amesema Waziri Mhagama

Pia amewasisitiza kufanya kazi kwa umoja, ushirikiano, bidii, weledi na kuendeleza utamaduni wa kukutana kwa lengo la kuboresha utendaji kazi kwa manufaa ya Taifa.

Pia amewaomba watumishi hao kutumia muda wao wa kazi vizuri ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu waliyopewa kwa ufanisi na kujituma ili kufanya kazi kwa viwango vya juu na kufikia malengo yaliyowekwa na ofisi pamoja na kutimiza ndoto zao binafsi katika utumishi.

“Msiweke matabaka na jitahidini kuepukana na migongano na migogoro mahali pa kazi ili kuleta tijja na upande wa menejimenti nawahimiza kusimamia ipasavyo utendaji wa wafanyakazi na upatikanaji wa haki na maslahi yao,” amesisitiza Mhagama