December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Mhagama atoa wito kwa wenye viwanda nchini

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Uratibu,Kazi, Vijana,Ajira naWenye Ulemavu) Jenista Mhagama ametoa wito kwa wenye viwanda nchini kuimarisha mifumo ya kulinda afya na usalama wa wafanyakazi ili kuleta tija katika uzalishaji na ukuaji wa biashara zao.

Ametoa wito huo alipofanya ziara katika kiwanda Cha Alaf Limited kinachozalisha mabati na bidhaa nyinginezo za chuma pamoja na kiwanda Cha kioo Limited kinachozalisha bidhaa mbalimbali za vioo, viwanda hivyo vipo Manispaa yaTemeke katikaMkoa wa Dar es salaam.

Katika maelekezo yake swali kwa menejiment za viwanda husika, Waziri Mhagama alieleza kwamba dhumuni la ziara yake ilikuwa ni kuangalia jinsi  viwanda hivyo vinavyozingatia masuala ya usalama na afya kwa wafanyakazi pamoja na masuala mengine yanayohusu Kazi ikiwani sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Kama walivyoeleza katika taarifa yao kiwanda hiki kina miaka 61 tangu kilipoanzishwa na serikali yetu ni mbia wa kiwanda hiki hivyo tunapoadhimisha miaka 60 ya Uhuru tumeona ni vema tukatembelea kiwanda hiki ili tuweze kuona katika kipindi chore kiwanda kimepata mafanikio gani?,” amesema Mhagama na kuongeza:

“Kupitia taarifa iliyowasilishwa na viongozi pamoja na Yale niliyoyaona nilipotembelea maeneo tofauti katika viwanda hivi nimefarijika kuona wamefanikiwa katika mambo mengi ikiwemo kuimarisha mifumo ya usalama na afya kwa wafanyakazi, maslahiya wafanyakazi yameendelea kuboreshwa kupitia uwepo mikataba ya hali bora,Aisha nimeiona kiwango cha kodi mnachochangia kwenye mapato na MFUKO Mkuu wa serikali ni kikubwa ambapo kea upande wa Araf Limited kea miaka mitano iliyopita kiwanda kimechangia zaidi ya bilioni  290 kiwango ambacho kinaridhisha.”

Katika ziara hiyo,viongozi wa viwanda vyote viwili walipatafursa ya kuwasilisha taarifa fupi kuhusu utendaji wao,mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika uzalishaji ambapo miongoni mwa mafanikio yaliyoelezwa ni pamoja na kutoa Ajira za moja kwa moja zipatazo 500 kwa kila kiwanda pamoja na kuchangia kodi kea ajili ya maendeleo ya nchi.

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama aliambatana na Mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pakazi (OSHA) Khadija Mwenda pamoja na watendaji wengine wa OSHA ambapo Bi Mwenda amewapongeza viongozi wa viwanda vya Araf Limited na Kioo Limited kwa kushirikia vema na Taasisi yake katika kuweka mifumo madhubuti ya kulinda nguvu Kazi suala ambapo ndio jukumu na msingi la OSHA.

“Kwa kweli wote mliojumuika nasi katika ziara hiii mmejionea jinsi viwanda hivi vilivyoweka mifumo mizuri ya kulinda afya na usalama wa wafanyakazi hivyo nawapongeza Sana wenye viwanda hivi kwa kushirikia nasi katika kutimiza wajibu wetu wa kuwalinda wafanyakazi pamoja na kulinda mitaji ya wawekezaji dhidi ya majanga mbalimbali. Aisha nawaahidi tu kwamba tutaendelea kushirikiana nao kwani jukumu letu ni kuwawezesha wawekezaji na sio kuwakwamisha katika shughuli zao za uzalishaji,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda.

“Alaf ni kampuni kubwa ambayo Ina miaka 61 Sasa tunatarajia itaendelea kukua zaidi hadi kufikia miaka 120 na zaidi na pia napenda kusema kwamba tumefarijika Sana Mhe.Waziri Mhagama kea kututembelea ili kujua mafanikio na changamoto zetu na hivyo kutusaidia  kuzitatua,” amesema Ashish Mistry Mkurugenzi Mkuu wa Alaf Limited.

Kwa upande wa Meneja Rasilimali Watu wa Kioo Limited, Jacob Msuya, ameishukuru OSHA kea kuwapa miongozo ya mara kea mara kuhusu uzingatiaji wa viwango vya usalama na afya Mahali pakazihusisan kupitia mfumo mpya wa kieletroki wa usimamizi wa maeneo ya Kazi ujulikanao kama WIMS yaani Workplace Information Management System ambao alieleza kwamba umeiondoa urasimu wa huduma za OSHA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira naWenye Jenista Mhagama (Mb), akizugumza na wawekezaji wa kiwanda Cha Kioo Limited kilichopo Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam alipofanya ziara aliambatana na baadhi ya viongozi wa OSHA kwa lengo la kukagua mifumo ya usalama na afya na kuangalia utekelezaji wa sheria Na 5 ya usalama na afya Mahali pakazi ya mwaka 2003.