November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Maryprisca aagiza mamlaka za maji kupanda miti

Na Esther Macha, TimesMajira Online,Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi(MB)Maryprisca Mahundi ameagiza Mamlaka za maji nchini kupanda miti milioni sita ikiwa ni utekelezaji wa sera ya utunzaji mazingira katika vyanzo vya Maji na kuiga mfano wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya wa kupanda idadi hiyo ya miti kwa mwaka 2020/21.

Mhandisi Mahundi amesema hayo jana wakati wa uzinduazi wa zoezi la la upandaji miti kwa mwaka 2020/2021.

Naibu waziri huyo amesema kuwa mamlaka zingine za maji zipande miti kwani vyanzo vya maji vina uwezo wa kubaki salama.

“Naagiza mamlaka zote za maji nchini kupada miti kwenye mikoa yao mkiweza kupanda miti mil.6 kwenye vyanzo vyetu hakika vyanzo vyote vitakuwa salama ,tuige mfano mzuri wa mamlaka maji Jijini Mbeya jinsi ilivyoweza kufanikisha zoezi hili ,kupitia zoezi hili linalofanyika mamlaka ya maji mbeya naamini miti ikipanda kwenye vyanzo vyetu vitakuwa katika hali ya usalama”amesema mhandisi Mahundi.

Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akipanda mti ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti.

Akielezea zaidi Mhandisi Mahudi amesema kuwa namna ambavyo vyanzo vya maji vinatunzwa hivyo Mkurugenzi wa mamlaka na watumishi wahakikishe kuwa miundo mbinu ya maji iendelee kuwafikia wananchi na kwamba asimilia inayowafikia ni asilimilia 50 tu na kwamba inamaana asilimia 50 ya wakazi wa Mbeya hawana maji na kwamba hakuna sababu ya kutesa asilimilia kubwa ya wananchi wasio na maji .

Hata hivyo ameutaka uongozi wa mamlaka ya maji wahakikishe wanajituma ili wananchi wawewze kupata maji safi na salama kwa asilimia 85 mpaka 90 na hiyo ndo adhma ya serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya maji ya mamlaka ya maji Jijini Mbeya ,Edina Mwaigomole amesema kuwa suala la utunzaji wa vyanzo vya maji wanalitambua wataendelea kuhakikisaha vyanzo vinalindwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuedelea kupanda miti.

Diwani wa Kata ya Mwakibete ,Lucas Mwampiki amesema kuwa kuna changamoto zipo kwenye vyanzo ambalo linahitaji ulinzi kwa kushirikiaa na wananchi ,na kusema kuwa licha ya kata hiyo kuzungukwa na chanzo cha maji lakini bado suala la maji ni shida hivyo ameomba watu wa idara ya maji kuwasaidia.