Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
SERIKALI ya Awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini ili kuweza kuwekeza kwa lengo la kuzalisha fursa kwa jamii na kufungua nchi katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa duka la “GADGET” leo Novemba 18, 2022 Masaka jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati Mheshimiwa January Makamba amesema kuwa anampongeza mmiliki wa duka hilo kwa sababu moja ya changamoto kubwa katika matumizi vifaa vya umeme nchini ni kutokuwa na ubora, kujitokeza kwa muwekezaji kama huyu ni fursa kwa wananchi kununua vifaa ambavyo vitakuwa na thamani ya fedha wanayotoa.
“Duka kama hili watu wengi wanapata ajira hapa na kulipa kodi kwa kiasi kikubwa kwahiyo ni kitu kizuri tumekuja kumuunga mkono kwa sababu siku zote nimekuwa nikinunua vitu kwake kama simu, chaji na nilivyosikia amefanya jambo kubwa kama hili nimeona nimuunge mkono na kumpongeza imani yangu ni kwamba mafanikio haya yataendelea na wateja wengi watanufaika, hivyo hakuna haja ya kuagiza tena vitu kutoka ulaya” amesema Makamba
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa amesema kuwa jambo kubwa ni kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuweka mazingira salama na wezeshi kwa wawekezaji ili kuwekeza, wafanya biashara wanauhuru wa kufungua maduka makubwa na kupelekea ajira na fursa nyingi kwa vijana na kuchangia uchumi kwa kiwango kikubwa.
“juzi ulisikia TRA sasa hawakusanyi kodi kwa “TASK FORCE” kodi sasa ni kwa wafanyabiashara kwa ‘accesiment’ niseme ni pongezi kwa serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuifungua nchi kwa kuendelea kuweka mazingira salama kwa wawekezaji kujitanua kama ilivyo kwa mmiliki wa ‘GADGET SHOP’ ameongezea kuwa
“Hivyo ni waambie watanzania wenzangu duka hili lipo wazi nalinatoa huduma bora hapa nchini, watumia fursa hii kuweza kufika ili kupata bidhaa bora na zauhakika kwa matumizi yao kama ilivyo kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifika hapa na kuacha kwenda kuagiza nje ya nchi” amesema Mbunge Jerry Silaa
Naye Mmiliki wa duka la GUDGET Zelfa amesema vijana wengi siku hizi wanasoma teknoloji hivyo ni fursa kwa vijana kujitokeza kwa wingi ili kupata ajira kwa sababu bado tuna changamoto ya wafanyakazi na tunahitaji watu, “sisi tunauza bidhaa kwa bei nafuu na rafiki kwa kila mtanzania na hatununui bidhaa hovyo hovyo huku dubai bali tunanunua kwa watengezeji wa hizi bidhaa” amesema Zelfa
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa