December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Makamba akutana na Waziri Sears

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amekutana na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Alfred M. Sears pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaoendelea jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 15 hadi 20 Januari 2024.

Katika kikao hicho, Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, biashara na Uwekezaji, michezo na utamaduni .