Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula,ametoa sadaka kwa waumini 882,wa dini ya kiislamu na kikristo waliopo Jimboni Ilemela.
Ikiwa ni kuwaunga mkono waumini wa dini hizo ambapo kwa waislamu kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kwa wakristu kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo(Pasaka).
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa sadaka hiyo lililofanyika shule ya msingi Kitangiri, Dkt.Angeline amesema,ametoa mchele,mafuta,sukari,ngano na tende kwa makundi maalumu yaliopo katika Wilaya ya Ilemela ambayo ni wazee,wajane na yatima.
“Tunatambua kuwa mwaka huu umekuwa mwaka wa baraka na neema tele,kwamba funga ya Ramadhani imekwenda sambamba na funga ya Kwaresima, leo ikanipendeza nikasema nije niwaunge mkono angalau kwa kusogeza siku ambazo zitakuwa zimebaki hata kama hazita fika lakini tutakuwa tutapunguza makali kidogo,”amesema Dkt.Angeline na kuongeza kuwa
Dkt.Angeline amesema wanatoa kwa misikiti 38 kwa makundi maalumu ya wazee,yatima na wajane,wanatambua changamoto iliopo lakini Rais Samia ametoa kauli kuwa tunapokuwa katika funga wanamambo mengi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuombea nchi.
Katika harakati ambazo wanaendelea nazo wote mnatambua kuwa bei za bidhaa ni kubwa lakini hali halisi ya kidunia imechangia kuwa na bei kubwa lakini serikali kupitia Waziri Mkuu ameisha toa tamko akiwaelekeza wafanyabiashara kutotumia fursa ya vita inayoendelea nchini Ukrein kama sababu ya kupandisha bei za bidhaa.
Kwa upande wake Johari Shabani,mmoja wa yatima walioipata fursa ya kupokea sadaka hiyo,amemshukuru Dkt.Angeline kwa kuwapatia sadaka hiyo,hivyo wanamuomba kwa Mungu aendelee kuwa na moyo wa kujitoa kwa ajili ya wahitaji.
More Stories
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha
Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla