Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Manaibu wake, Mhe. Cosato Chumi (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dennis Londo (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki; wamefanya ziara ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.
Katika utambulisho huo, viongozi hao wamemuhakikishia Rais Mwinyi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuhakikisha kuwa maslahi ya pande zote mbili—Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar—yanapewa kipaumbele. Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Wizara ya Muungano.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto