December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Jafo atoa maagizo TIRDO

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Waziri wa viwanda Dkt. Selemani Jafo ameutaka uongozi wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kuhakikisha kabla ya mwezi wa tano mwakani wanatembelea mikoa yote 26 kubainisha nchi ina viwanda vingapi vilivyojengwa na vinavyofanya kazi.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara na kukagua namna shirika hilo linavyofnaya kazi ambapo aliwapongeza kwa kuwa na mfumo wa digitali wa kutambua viwanda nchini ambao mpaka sasa umeshafanya kazi katika mikoa mitano ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Arusha ja Kilimanjaro huku akiahidi hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu kuuzindua rasmi mfumo huo.

“Kabla ya mwakani mwezi wa tano nataka muende mkafanye kazi tuweze kumaliza mikoa yote kubainisha jinsi gani tuna viwanda hivi nchini mwetu vilivyojengwa na vinavyofanya kazi, watu waende SITE wasikae ofisini mgawane katika mikoa mbalimbali chini ya mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA”

“Wekeni utaratibu wa jinsi gani tutafanya mwaka huu utakapoisha tuwe tumekamilisha tupate idadi ya viwanda vyote nchini Tanzania watu waende site wasikae ofisini mgawane katika mikoa mbalimbali chini ya kkurugenzi wa idara ya TEHAMA” Alisema Waziri jafo na kuongeza kuwa;

“Niwapongeze kwenye mfumo wa kidigitali wa kutambua viwanda vyetu nchini , nimefarijika sana na mfumo ule nimeambiwa mmefanikiwa kufanya kazi hii katika mikoa mitano Dar es salaam, Pwani, morogoro na mikoa miwili katika kanda ya kaskazini Arusha na Kilimanjaro”

Aidha Waziri Jafo amewaagiza TIRDO kutenga kitengo maalumu cha kutafuta fedha ili kusaidia taasisi kusonga mbele na kuwafanya vijana wawe wanajishughulisha na kazi hasa katika kufanya tafiti mbalimbali.

Kadhalika Waziri Jafo amewataka TIRDO kuorodhesha miradi yote ya maendeleo .

“Mwaka jana nilizindua mradi kutoka Norwey mbona sisi TIRDO hatujachangamkia hiyo fursa? Tunataka TIRDO iliyo simama na watu wanasonga mbele”

Pia amewataka TIRDO kujali muda katika majukumu yao ili Taasisi iweze kuwa hai muda wote

“Jalini muda, fanyeni kazi kwa muda, pangeni mambo yenu kwa malengo na mtimize mambo yenu kwa muda mliojiwekea ili taasisi iwe ‘active’ sana”