Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wajane kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kujiunga katika vikundi na taasisi za kuwawezesha kiuchumi, kuepuka, umaskini na utegemezi katika jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha Wajane jijini Dar es salaam Waziri Gwajima amesema Serikali haitafumbia macho yeyote anayemnyanyasa mjane au kumdhulumu haki yake, hivyo kwa wale wanaofanya amewataka kuacha mara moja.
“Msiogope kujiunga katika vikundi na taasisi za kuwawezesha kiuchumi, kuna majukwaa ya kuwawezesha wananchi kiuchumi” amesema Waziri Gwajima
Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kuandika wosia ili kuepusha migogoro ndani ya familia kwa sababu inaathiri wajane na watoto.
Hivyo, Dkt. Gwajima amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa wajane.
More Stories
Mwabukusi:Kufanyakazi kwa kushirikiana na serikali siyo kulamba asali
Waislamu wamuombea dua Rais Samia,wasisitiza umoja
Samia: Serikali imejifunza somo kuporomoka ghorofa