Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imepata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum – Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Ruth Zaipuna aliembatana na Afisa Mkuu wa Fedha NMB – Juma Kimori, amempokea Mhe. Gwajima na kumuelezea kuhusu masuluhisho yanayogusa moja kwa moja makundi mbalimbali katika jamii.
Lakini pia, aliahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha masuluhisho yao yanakuwa chachu ya maendeleo kwa makundi yote katika jamii kwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia na ubunifu.
Katika salamu zake, Mhe. Gwajima alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wetu pamoja na uongozi mzima wa Benki wa NMB kwa mafanikio waliyoyapata, na kuahidi kuna balozi mzuri kufikisha fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi ili waweze kujijenga kiuchumi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba