Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam isipikuwa maeneo yakiyoainishwa.
“Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling (kushughulikia) ya jambo lenyewe. Serikali yetu ya Awamu ya Sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao.” amesema Bashungwa
” Namuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi.”
Tangazo la kusitisha vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya Jiji lilitolewa tarehe 20.04.2022
More Stories
CP.Wakulyamba ashuka Katavi na Nguzo nne za Uongozi
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto