Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Siku tatu tangu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo kuagiza wizara ya kilimo kusikiliza kero za wakulima mkoani Morogoro, Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe leo Februari 4, ameanza ziara ya siku mbili mkoani Morogoro na kutoa maagizo yanayolenga kutatua kero za wakulima.
Kati ya maagizo hayo ni pamoja na kuagiza kujengwa ukuta kuzunguka skimu ya umwagiliaji ya Uwawakuda iliyopo Dakawa.
Waziri Bashe akiwa kwenye skimu hiyo amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima wakiongozwa na Diwani wao Yusuph Makunja ambaye amelalamikia uuzwaji wa kiholela wa maeneo kwenye simu hiyo ukiwemo uwanja wa ndege ambao umekuwa unatumiwa na ndege za kunyunyizia dawa ya kuua wadudu waharibifu wa mazao.
Eneo hilo lina ukubwa wa hekari 3225 ambapo hekari 2000 zinaendelezwa, hekari 1000 huku hekari 225 zikitumiwa kwa ajili ya makazi ya watu.
Waziri Bashe amesema haiwezekani maeneo ambayo yanatakiwa kutumika kwa ajili ya shughuli za kilimo kuuzwa na kumilikiwa na watu wachache huku wengi ambao ni wakulima wakiachwa bila ya maeneo.
Ameagiza kujengwa ukuta kuzunguka eneo zima la simu hiyo huku akimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma kuhakikisha waliouziwa maeneo wanarejesha kwa wakulima.
” Yani haiwezekani eneo ambalo linatakiwa kutumika kwa shughuli za kilimo lakini linachukuliwa na watu wachache nakuagiza Mkuu wa Mkoa ufuatilie suala hili na mkandarasi atakuja hapa kujenga ukuta ili kulinda eneo hili kushutumiwa” amesema Waziri Bashe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Lyasa amemesema kuwa kumekuwa na uuzwaji wa ardhi kiholela wilaya ya Mvomelo hadi kufikia hatua ya kutaka kuuza ardhi ya yaliyopo makazi ya Mkuu wa Wilaya.
Akiwa katika Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe leo Februari 4, ameanza ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Morogoro na kutoa maagizo kadhaa yanayolenga kuimarisha kilimo. Katika ziara hiyo aliyoongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Lyasa na watendaji wengine wa mkoani na wa Wizara ya Kilimo.
Akiwa katika Skimu Uwahulu iliyopo Kijiji cha Wami Luhindo wilayani Mvomero, Waziri Bashe amewataka wananchi kuacha kuuza ardhi yao badala yake waitumie kwa shughuli za kilimo na kunufaika na uwekezaji unaofanywa na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan katika kilimo.
“Tatizo kubwa la wananchi wa Morogoro ni kuuza ardhi, utakuta watu kutoka Dar es Salaam ndiyo wanamiliki ardhi sehemu kadhaa hapa mkoani, hivi baada ya miaka kadhaa ijayo hawa watoto wenu watapata ardhi za kulima”
Waziri Bashe akiwa kwenye skimu hiyo ya umwagiliaji ameagiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha eneo hilo linapatiwa hati miliki na wakulima 488 wanaofanya shughuli za kilimo katika skimu hiyo kupatiwa hati ndogo ya umiliki huku akipiga marufuku eneo hilo kutumiwa kama dhamana ya kuchukulia mikopo.
Waziri Bashe amesisitiza kuwa hatoruhusu siasa katika shughuli za kilimo na kuwa hatoacha kuchukua hatua kali kwa watendaji ambao wanarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuendeleza kilimo nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Fatma Mwasa amewahakikishia wananchi katika elimu hiyo kuwa serikali ya Mkoa itasimamia kwa umakini ugawaji wa ardhi kwa wananchi wote na watakaonufaika ni wale wanaostahili tu
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu