Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii , Balozi Dkt. Pindi Chana alipokuwa akitoa salamu za Wizara wakati wa kufunga Maonesho ya Utalii Karibu Kusini mkoani Iringa.
Amesema Tanzania hususani mikoa ya Kusini ina maeneo mengi yenye vivutio vya Utalii ambayo ni vya kipekee duniani kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya Tembo na wanyamapori wengine, Hifadhi ya Taifa ya Kitulo yenye aina mbalimbali za maua, Utamaduni na vingine vingi.
Aidha Balozi Dkt Chana amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa kumtuma Makamu wake wa Kwanza wa Rais Othman Masoud amwakilishe kufunga maonesho hayo ambayo ni moja ya zao la Utalii la mikoa ya Kusini.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â