Na Mwandishi wetu,timesmajira
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana ameweka Kambi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni mwendelezo wa ushiriki wake kuhakikisha moto unaowaka katika maeneo machache yaliyosalia katika hifadhi ya Mlima huo.
Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Chana amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi inayoendelea ya kuzima moto akiwashukuru na kuwapongeza wadau wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha moto unadhibitiwa katika maeneo yote.
Balozi Dkt. Chana ameendelea kukemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaoanzisha au kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuisababishia Serikali na wananchi wake hasara kubwa akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

“Huu ni msimu wa maandalizi ya kilimo, natoa rai kwa ndugu zangu wakulima mnaopakana na Hifadhi za Taifa muwe makini pindi mnaposafisha mashamba yenu, msitumie moto bali tafuteni njia mbadala ili kuepusha moto kuchoma Misitu na kusababisha hasara kubwa, yeyote atakayesababisha moto kwenye Hifadhi za Taifa atachukuliwa hatua kali za kisheria”. Amesisitiza Balozi. Dkt. Chana
More Stories
Rais Samia amrudisha January kwa Mama,asema kilichotokea ni kumuonya
Milioni 236 kunufaisha vikundi 17 vya wanawake Minazi Mirefu
Mipango 10 kabambe ya TPA