Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Mwanza
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewataka mameneja wa Mamlaka za Maji nchini kuwaeleza Mameneja Masoko wenu wasiwape wasoma mita malengo ya makubwa ya makusanyo yasiyo halisia ambayo hayatekelezeki na yanawaumiza wananchi na kusababisha malalamiko.
Badala yake aliwata mameneja hao wasimamie kikamilifu zoezi la usomaji wa mita za maji ziwe halisia ili kuepuka kuwabambikia wananchi bili za maji.
Aweso amesema ni haki ya mwananchi kupatiwa huduma ya maji naye wajibu wake kulipa bili za maji lakini zisiwe bambikizi kwao.
Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mradi wa Maji wa Buswelo ambapo aliwaelekeza Mameneja Masoko hao kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala za usomaji wa mita za maji ili kuepusha malalamiko.
“Baadhi ya maeneo wananchi hulalamikia bili za maji naomba wakurugenzi waelekeze mameneja masoko wenu wasiwape malengo makubwa ya makusanyo wasoma mita yasiyohalisia maana leo unampa malengo makubwa ya makusanyo hafikii atakachokifanya atambambikizia bili mwananchi ili akuridhishe hivyo wekeni makarido halisia” amesema .
Hata hivyo amewataka wahakikisha wanaweka makadirio halisia juu ya kukusanya mapato ili wananchi waweze kulipa bili stahiki ambazo sio kichefuchefu.
Katika hatua nyengine amewataka Wakala wa Maji Vijijini RUWASA na Mamlaka ya Maji ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza kuhakikisha tenki lililopo eneo la Igogwe na kahama tokea 2017 ambalo hakuna usambaji wowote wa huduma maji wajipange miradi hiyo waende kuikamilisha na wananchi wapate huduma za maji.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi