Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbeya
KUTOKANA na uhalibifu wa mazingira wa ukataji miti ovyo na uchomaji moto wazee wa mila wameiomba serikali iwapatie mlima mwene uliopo katika wilaya ya chunya mkoani hapa ili waweze kuulinda na kuutuza ili kuepukana na uharibifu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara hali ambayo imesababisha kupotea kwa uoto wa asili katika mlima huo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mzee wa mila ,Emmanuel Delecho wakati alipokuwa akiongea na baadhi ya viongozi wa serikali katika mlima huo ambao umezungukwa na kata ya Mamba kijiji cha Mtande wilayani humo ameiomba serikali iwapatie hifadhi ya mlima huo kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika eneo hilo.
Ombi hilo limekumeja kutokana na madai ya kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakiwadharau wazee pindi wanapokuwa wanaambiwa juu ya kuhifadhi mazigira katika mlima huo.
“Baadhi ya vijana wamekuwa wakitudharau sisi wazee pindi tunapowaeleza juu ya uhifadhi wa mlima huu tumekuwa tukipokea maneno ya kejeri kwao hivyo tungeomba serikali itupatie huu mlima ili tuweze kuulinda vizuri”amesema .
Mzee mwingine wa Mila , Athumani Mwakipesile amesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakijitahidi kuulinda mlima huo licha ukataji miti ovyo kuendelea na uchomaji moto ,mlima huu ni muhimu lakini unaenda kupoteza uoto wake kutokana na hali halisi iliyopo .
Mmoja wa wananchi wa eneo hilo ,Romanus James amesema kuwa wazee wa mila waliopo eneo hilo wamekuwa msaada mkubwa katika kuulinda mlima huo licha ya baadhi ya watu kuendelea kuvamia na kufanya uharibifu wa mazingira ambao kwa baadaye ni kuja kupoteza uoto wa asili.
Ofisa Utalii wilaya ya chunya ,Petro Haule amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana vema na wazee wa mila ili kuendelea kuulinda mlima huo ambao unatumika katika shughuli za matambiko ya wazee hao pia amewataka wadau na watalii kujenga tabia ya kuwa wapenda kutembelea katika mlima huo kwani una vivutio vingi ikiwembo kaburi la chifu mwene na msaidizi wake na mapango mengi ambayo yanapatikana katika mlima huo .
“Hawa wazee wamekuwa msaada mkubwa sana kwetu hivyo tungeomba jamii hasa vijana ambao wanajishughulisha na uchomaji mkaa na ukataji miti ovyo kuona kazi kubwa inayofanywa na wazee wetu hao “amesema Haule.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba