December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazee Mbeya wampongeza Dkt.Tulia kwa kujali wenye uhitaji

Na Esther Macha,TimemajiraOnline, Mbeya

BAADHI ya wazee Jijini Mbeya wamempongeza Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Rais umoja wa mabunge duniani Dkt.Tulia Ackson kwa namna anavyo jitoa katika kusaidia makundi mbalimbali ya watu wasiojiweza ikiwemo wazee.

Akizungumza na Timesmajira mmoja wa wazee hao, Ester Thomas mkazi wa Majengo mkoani Mbeya amesema kuwa Dkt.Tulia amekuwa mtu wa tofauti kwa jamii bila kujali itikadi za vyama katika kusaidia wananchi wasiojiweza na watu wanaoishi katika mazingira magumu hasa utoaji bima za afya kwa wazee.

“Unajua mfano sisi wazee tulio wengi hatuna uwezo lakini amekuwa akitukumbuka mara kwa mara hasa kwenye eneo la bima za afya ameweza kutukatia wazee hivi sasa hatupati shida kwenye matibabu tunamwombea Mh. Dkt.Tulia”amesema .

Mzee mwingine mkazi wa sokomatola mkoani Mbeya,Maria Panja amesema kuwa wazee walio wengi wamekuwa na maisha ambayo baadhi yao yanawafanya kukosa matibabu mara wanapougua lakini kwa Mh.Dkt.Tulia kuwakumbuka wazee kuwakatia bima kinaleta faraja kubwa kwao maana eneo la matibabu ni muhimu kwa wazee .

“Wazee tulio wengi tunapitia mambo mengi hasa umri tulio nao una mengi sana hivyo sisi wazee tumeona anachofanya kiongozi huyu ni chema kwetu tunapaswa kumpongeza maana tuna viongozi wengi wanaojali ni wachache “amesema.

Eda Siamba Ambaye ni mnufaika wa Bima ya Afya zilizotolewa na Dkt,Tulia akson amesema kutokana na Bima hiyo imemuwezesha kupata matibabu pasipo na changamoto yoyote.

Aidha Diwani wa kata ya Iyela Mussa Ismail amesema Dkt,Tulia amefanyika Baraka kwa wananchi wa jiji la Mbeya na nje ya jiji la Mbeya kutokana na kuwa na moyo wa upendo kwa kila Mwananchi katika kusaidia makundi Mbalimbali.

Aidha Diwani Ismail amesema Mh.Dkt.Tulia amekuwa kimbilio la makundi mbali mbali ambayo yamekuwa yakipatwa na changamoto za kimaisha hususani kundi la wazee ,watoto na familia zisizojiweza kwa kutoa mahitaji na wengine kujengewa nyumba”amesema.

Kwa upande wake Ofisa Habari na Masawaliano wa Taasisi ya Tulia Trust,Joshua Mwakanolo amesema kuwa mpaka sasa wameweza kutoa bima za afya kwa wazee waliopatiwa bima za afya ni zaidi ya watu 16,000 wakiwemo wazee na rika zingine pamoja na wanao ishi kwenye mazingira magumu zaidi.

Aidha Mwakanolo amebainisha kuwa ndani ya mkoa wa Mbeya wana mkakati wa kuwajengea nyumba wazee 181 wanao ishi kwenye mazingira magumu zaidi hapo ni kila mtaa walau mzee mmoja aguswe katika kufanikisha ujenzi wa nyumba za wazee wanaoishi katika mazingira magumu.

“Tunatamani sana kufikia kila kona ya Tanzania, kuhusu bima za afya tunatamani kuwafikia wazee na watu wasio jiweza ndani ya Jiji la Mbeya ikiwa ni pamoja na kuweka mpango maalum utakao saidia kuwapatia vyakula pamoja na mavazi.

Akielezea zaidi kuhusu Mh.Dkt.Tulia amesemsa kuwa anatamani kuona watu wakipata tumaini jipya kwa kuwa na furaha kama vile sisi wengine tulivyo na amani na maisha yetu na Mh hatamani kuona watu wana lala njaa na kukosa huduma muhimu kama za afya, pia anatamani kuona wazee wanathaminika zaidi kwenye jamii zetu.

Mmoja wa wazee akikabidhiwa kadi ya bima ya afya na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati,Dkt.Dotto Biteko kadi hizo zikitolewa na Dkt Tulia Ackson ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani
Baadhi ya wazee walioshiriki zoezi la ugawaji wa kadi za bima za wazee ambazo zilitolewa na Dkt.Tulia.