January 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na wasiojiweza Sukamnahela wakisubiri kupokea msaada wa vitu mbali mbali vilivyotolewa na Wizara ya Afya.

Waze 281 wanaoishi kwenye makazi wapewa matunzo

Na Jumbe Ismailly, TimesMajira Oline,Manyoni

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto,Dkt John Jingu amesema wazee 281 wanaoishsi katika makazi 13 ya wazee nchini wakiwemo wanaume 161 na wanawake 120 wamekuwa wakipatiwa kikamilifu matunzo katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari,hadi kufikia mwezi septemba,mwaka huu.

Baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na wasiojiweza Sukamnahela wakisubiri kupokea msaada wa vitu mbali mbali vilivyotolewa na wizara ya afya.

Akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwenye makazi ya wazee na wasiojiweza Sukamahela,Kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng’ondi alisema kwamba kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003,inatambua wazi kwamba wazee ni raslimali muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo Dkt.Jingu amebainisha kuwa makazi ya wazee ya Sukamahela kuna jumla ya wazee 15 wakiwemo wanaume 12 na wanawake 3 na kwamba kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto inajivunia kupata mafanikio katika maeneo mbali mbali ya utoaji wa huduma kwa wazee.

“Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya mwaka 2003 inatambua kuwa wazee ni raslimali muhimu kwa maendeleo ya taifa,hivyo ili kulinda haki na ustawi wa wazee,sera hiyo inatoa jukumu kwa familia na jamii kuchukua jukumu la kutoa matunzo kwa wazee” amesisitiza.

Aidha Dkt.Jingu amebainisha kwamba kwa wazee ambao wamekosa ndugu na jamaa wa kuwatunza, Serikali imekuwa ikichukua jukumu la kuwataunza wazee hao katika Makazi mbali mbali nchini.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kuboresha miundombinu na majengo ya makazi ya wazee kwa kufanya ukarabati na ujenzi mpya na kwamba miongoni mwa makazi yaliyoboreshwa ni pamoja na makazi ya Sukamahela.

Hata hivyo Dkt.Jingu amesisitiza kwamba makazi ya wazee na wasiojiweza Sukamahela yalianzishwa mwaka 1974 na lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kutoa huduma za matibabu pamoja na huduma zingine za msingi kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukoma na familia zao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi (aliyevaa miwani) akimkabidhi mwenyekiti wa wazee wanaoishi kwenye kambi ya wazee na wasiojiweza Sukamahela vifaa mbalimbali ili viweze kuwasaidia katika mahitaji yao.Picha zote Na Jumbe Ismailly

Akikabidhi msaada wa vitu mbali mbali kwenye makazi ya wazee na wasiojiweza,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Rehema Nchimbi amewahakikishiwa wazee hao kwamba Serikali inawapenda sana na ndiyo maana ofisi itakayoendelea kuwahudumia kikamilifu ikafunguliwa kwenye Makazi hayo