November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazazi watakiwa kushirikiana na walimu kwenye malezi ya watoto

Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Wito umetolewa kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na walimu katika suala zima la kulea watoto na kuachana na dhana potofu kuwa walimu pekee ndio wanatakiwa kuwasimamia katika suala zima la maadili

Kwa sasa jamii imebadilika sana tofauti na hapo awali ambapo wazazi wengi wanawaza suala zima la ada pekee na kuona kuwa ndio kipaumbele

Hayo Yameelezwa na meneja wa shule ya awali pamoja na msingi y Arusha Victory kwenye mahafali ya nane ya darasa la saba ambayo yamefanyika shuleni hapo wiki iliyopita

Kamwe alisema kuwa pamoja na kuwa maisha yanahitaji utafutaji mkubwa wa fedha na miradi lakini bado watoto wana nafasi kubwa sana ya kulelewa na wazazi kwa kuwa wasipowakari ipasavyo ndio chanzo cha maadili

Alifafanua kuwa wazazi wengine bado hufikiria kuwa wenye jukumu la kuhakikisha watoto wanakuwa na maadili mema ni walimu jambo ambalo sio la kweli.

“masuala ya majukumu ya ulezi sio ya walimu pekee bali ni pamoja na wazazi lazima tuhakikishe kuwa tunakuwa kitu kimoja na tunawalea kwa kushirikiana kwa umoja”aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa shule hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuhakikisha kuwa inawalea watoto katika njia nzuri yenye maadili lakini pia kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji.

“hapa shuleni tunalea na kuibua vipaji na vipaji ambavyo tunavilea vinaonekana nataka tu kuwaasa hata wazazi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na walimu katika kulea vipaji”