Na Bakari Lulela, Timesmajira Online
WAZAZI wa wahitimu wa shule ya awali ya Light Day Care Tandale jijini Dar es salaam, wametakiwa kuwapeleka watoto wao shuleni.
Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika ukumbi wa Tanhope ambapo jumla ya watoto 28 wamehitimu ngazi ya awali.
Akizungumza jijini mgeni rasmi katika mahafali hayo mwenyekiti wa serikali ya mitaa wa eneo la kwatumbo Hatibu Kibwana amesema watoto hao ni nguzo kubwa katika maisha ya baadae.
,,Mimi Kama mzazi nawashauri wazazi wenzangu tuwatendee haki watoto wetu hawa ya kupata ya masomo ngazi ya msingi,amesema kibwana
Kibwana amesema jukumu kubwa la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kujiunga na masomo ya msingi kwa wakati.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Nuru Rashid amewataka wazazi wasibweteke katika kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wawapo mashuleni.
Aisha mwalimu huyo amesema dunia hii ina changamoto nyingi lakini isiwe sababu ya kutowapeleka watoto hao mashuleni.
Nae mhitimu wa shule hiyo Abdul razaki Bakari amewapongeza walimu wake kwa hatua mbalimbali walizokuwa wakiwafundisha na kuahidi kufanya bidii zaidi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa