Na Pius Ntiga, TimesMajira Online, Siha
ZAIDI ya ajira 2,000 zimepatikana katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano kwa wananchi kufanyakazi katika miradi mbalimbali ukiwemo wa Shamba la Mwekezaji la Maparachichi-Africado.
Miradi hiyo mikubwa ya mwekezaji Africado lililopo Kijiji cha Kifufu pamoja na ule wa Shamba la uzalishaji wa mayai ya kisasa lenye ukubwa wa hekari 507 lililopo Kijiji cha Namwai, la Mwekezaji Irvine Family, imezalisha ajira zaidi ya 700 Kati ya 2,000 za wananchi kuanzia mwaka 2015-2020.
Akizungumza na Gazeti la Majira amesema kuwa miradi hiyo inalenga kuainisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli,Meneja Utawala wa Shamba la Africado,Berinda Meena, amesema shamba hilo limesaidia kupatikana kwa ajira 500 za wananchi wa Siha ambazo zimefanikisha kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato.
Chini ya mafanikio shamba hilo la Africado lenye uwekezaji wa mabilioni limekuwa likisaidia pia wafanyakazi kujengewa uwezo wa ujuzi wa kilimo kwa kufunga Vikonyo,ambapo sehemu kubwa ya wafanyakazi Wana mashamba yao binasfi.
Amesema wanyakazi hao wamekuwa wakipatiwa pembejeo bure na mwekezaji huyo ambapo mazao yao huyauza pia katika shamba ya huyo mwekezaji Africado ambapo mwekezaji wake ni James Pasoz raia wa Ujerumani.
“Tangu mwekezaji huyu awekeze katika shamba hilo ambapo sasa yapata miaka 10 wamekuwa wakizalisha maparachichi na kuyauza Ulaya na Uarabuni” amesema Berinda.
Kwa mwaka huu zaidi ya tani 3,600 amesema zimezalishwa katika shamba hilo na kuuza nje ya nchi.
“Maandalizi ya shamba la maparachichi ni miaka mitatu kuanzia hatua ya kupanda miche hadi kuvuna kwa kutumia mbegu ya hasi inayokuwa haraka” amesema.
Aidha,amesema Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa kutoa leseni kupitia EPZ na msamaha wa kodi na kuwezesha eneo kubwa kwa kuweka mtaji mkubwa, na hivyo ameipongeza Serikali kwa kumsaehe pia VAT kwa vitu anavyonunua kwa ajili ya shamba hilo.
Pia Berinda amesema mwekezaji huyo amekuwa na mahusiano mazuri kati yake na serikali.
Aidha,amesema mazingira ya uwekezaji sasa ni mazuri kwa kiasi kikubwa wamekuwa na mazingira ambayo yamesaidia kampuni hiyo kukuwa kwa kiasi kikubwa.
pia amesisitiza kuwa bado wanatafutwa maeneo mengine ya kuwekeza zaidi wilayani Siha.
“Shamba hilo limekuwa na msaada mkubwa kwani kipato kinachopatikana kimekuwa kikisaidia kukuza uchumi wao pamoja na kujenga shule ya msingi Karagoha na kutoa kampeni ya matibabu bure ya Macho” amesema.
Wakati huo huo,Meneja Mwendeshaji wa Shamba la Mayai ya Kisasa la Joseph Kasegama,amesema shamba hilo limepunguzaa upungufu uliokuwepo nchini wa upatikanaji wa vifaranga vya kuku na limesaidia ajira 120 za wananchi wa Siha na kuongeza pia mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
“Shamba hilo la Irvine Family lenye hekari 507 lina abanda 507 yenye uwezo wa kuchukua kuku 9,000” alisema.
Katika hatua nyingine,Mkuu wa Wilaya ya Siha,Onesmo Buswelu, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kupeleka kiasi kikubwa cha fedha za maendeleo katika wilaya hiyo ambazo pia zimewezesha kukarabati pia Hospitali ya Wilaya ya Siha.
Chini ya fedha hizo Hospitali ya Kibong’oto inayotibu pia watu wa Kifua Kikuu-TB, imepelekewa shilingi Bilioni-7 huku Hospitali ya Wilaya ya Siha imepokea shilingi Bilioni-2 zilizofanya ukarabati Mkubwa.
Aidha, amesema zaidi ya bilioni 50 zimetumika kujenga barabara za lami wilayani humo sanjari na kurahisisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na Salama.
Pia amesema mpango wa elimu bure umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi na sekondari wakiwemo wa jamii ya Kimasai.
“Ni kwamba Ukanda wa Kasikazini haujasaulika, kwani kumekuwa na maneno kuwa Ukanda huu umesahaurika kitu ambacho sio kweli” amesema.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea