December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wawaili mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa wawili Kwa tuhuma za mauaji ya Ndembora Exaud Nanyaro aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhumiwa na watuhumiwa hao mei 20, 2024 huko katika Kijiji cha Ngurudoto Kata ya Maji ya chai wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha mei 25,2024.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema marehemu alifariki dunia mei 25,2024 huko katika hospitali ya KCMC wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Jeshi la Polisi Mkoa Arusha linashikilia watuhumiwa hao wawili ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi na pindi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ulibaini kuwa chanzo cha shambulio hilo lililopekea mauaji hayo ni ugomvi wa wanandugu ambao Jeshi hilo limesema kuwa linaendelea na uchunguzi huo ili kubaini chanzo halisi cha mauaji hayo.

Jeshi la Polisi Mkoani humo limetoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria Mkonani na baadala yake wafike katika mamlaka zinazohusika ili kutatua changamoto zao ikiwa ni Pamoja na viongozi wa dini