Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Waumini wa Kanisa la ‘Halisi la Mungu Baba’ wakiongozwa na Mchungaji kiongozi ‘Baba Halisi’ ameongoza ibada maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu.
Ibada hiyo ilifanyika katika Uwanja wa Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kumtakia heri na baraka Rais huyo katika uongozi na utendaji wake katika kuliongoza Taifa la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar Kiongozi wa Kanisa hilo, Baba Halisi aliwataka viongozi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani Kanisa la Baba halisi limekuwa likiwaombea kwa utendaji wao.
“Tunatambua Mchango wenu na Changamoto mnazopitia lakini tunafanya maombi kwaajilinya Rais Samia Suluhu na viongozi wake wote wafanye kazi kwa amani Taifa likiwa na utulivu.” Alisema Baba Halisi
Pia aliongoza kuwa “Tumeambatana na kufanya usafi katika maeneo ya Tegeta Nyuki yote ni katika kufanya usafi wa roho lazima kuwepo na usafi wa mwili na mazingira.”
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule kama Wilaya kitu cha kwanza wanachotamani kiwepo ni hali ya amani, usalama, utulivu, na hivyi vimekua ni msingi wa kanisa la Halisi.
“Amani ni kitu namba Moja, tunafahamu pasipokuwepo na amani hakuna kitu kitafanyika, hakuna elimu, hakuna afya, hakuna ustawi, hakuna maendeleo, uchumi, mapato, Wala ajira, hivyo hongereni Wana Halisi kwa kufanya amani kuwa ni jambo la msingi kwenye kanisa hili halisi”
“Amani inaposisitizwa sehemu yoyote sisi serikali tunakua ni sehemu ya kushiriki kuhamasisha na kulinda amani ya maeneo yetu, lakini hili la upendo niwashukuru sana kwa jinsi ambavyo mnaendelea kutujenga kiroho, kutuhamasisha na kutuunganisha pamoja, na tunaiyona amani hii na upendo huu ambao umeendelea kuwepo”
Mtambule alisema Rais Samia anataka uimarishwaji zaidi katika amani, upendo, utulivu na kushiriki mambo mbalimbali katika jamii ya maendeleo.
“Tuendelee kuwa kitu kimoja, kuhubiri amani, upendo, tuendelee kuhubiri wananchi wetu wafanye mambo yaliyokuwa halisi”
Mtambule aliwaahidi Wana Halisi kuendelea kushirikiana nao katika majukumu yao ikiwemo uzalishaji wa bidhaa ambazo kanisani hapo ambazo zitaenda kuzalisha ajira, mapato na kukuza uchumi.
“Tutakuja kama kuna kitu Cha kufanya,shughuli hizi zinazofanywa hapa za uzalishaji kupitia kanisa hili,kama kuna kitu tunatakiwa tukifanye ili uzalishaji uwe mwingi na bora zaidi, tutakuja tushirikiane Tufanye hivyo, kwasababu tunatambua kupitia kazi kama hizo tutazalisha na kutengeneza ajira, mapato, wananchi wenye uchumi na ustawi mzuri zaidi na itatusaidia uagizaji wa kilakitu kutoka kwenye mataifa mengine”
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato