Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma
WAKAZI wa Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutumia vyema fursa zinazopatikana katika makao makuu ya nchi kutoka na Dodoma kuwa makao makuu na kuwepo na wageni wengi wanaoingia na kutoka.
Rai hiyo imetolewa na mchungaji kiongozi wa kanisa la Calvary Assembles Of God(CAG) Mlima wa Nuru lililopo mtaa wa Chamelo Nzuguni ‘B’Jijini Dodoma Silvester Kamara alipokuwa akiubiri katika ibada ya jumapili kanisani hapo.
Mchungaji Kamara amesema kuwa kwa sasa Dodoma ni makao makuu ya nchi na kuna wageni wengi wanaingua na kutoka hivyo ni vyema watu wakawekeza katika ununuzu wa ardhi hususani waumini wa kanisa hilo.
Ahubiri kanisani hapo amesema kuwa yapo mataifa mengi ambayo hayana ardhi ya kutosha na wanatamani kuipata lakini hawaipati hivyo ni wajibu wa wana Dodoma kuchangamkia fursa ya kupata umiliki wa ardhi bila kujali ardhi hiyo inapatikana wapi.
“Kuna mchungaji mmoja kutoka Jiji la Mwanza alinipigia simu akiniuliza ,vipi?huko Dodoma ardhi inapatikana? katika kumjibu nilimwambia kuwa kimsingi bado sijafuatilia kujua hali ya upatikanaji wa ardhi katika Mkoa wa Dodoma.
“Sasa unaweza kuona watu waliopo mbali wanapofikiria kuwekeza katika ardhi katika Mkoa wa Dodoma!hivyo nataka kuwaambia waumini kuwa wekeza zaidi katika kununua ardhi hata ukipata mita 50 kwa kwa 30 bila kujari unaoata kupata wapi bali hakikisha unapata hata kama utaona kuwa ni mbali kwa wakati huu”amesisitiza Mchungaji Kamara.
Mchungaji Kamara amesukumwa kuwahamasisha washirika wake kuwekeza katika ununuzi wa ardhi katika Mkoa wa Dodoma kutokana na wageni wengi kutoka mikoa mbalimbali kuchangamkia fursa mbalimbali huku wenyeji wakiendelea kushangaa.
Kwa sasa kuna Dodoma kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kuwafanya watu kujipatia kipato pindi watachangamkia fursa mbalimbali.
Kwa Dodoma kuna kiwanda kiwanda kikubwa cha kutengeneza Mbolea,kituo kukubwa cha reli ya kisasa kiitwacho Samia Station kilichopo mkonze ambacho kinapokea wageni au wasafiri zaidi ya 7000 kwa siku.
Katika hatua nyingine amesema kuwa kutokana na Dodoma kuwa na fursa nyingi kwa sasa kuna kila sababu ya kuuombea Mkoa wa Dodoma ili amani iweze kutawala na kuondokana na uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi.
Pia amehimiza watu wote wanaomwanini Mungu kuliombea taifa ili liepukane na majanga mbalimbali ya magonjwa kama inavyotajwa kwa sasa kuwepo kwa ugonjwa wa nyani.
Kuhusu masuala ya kiafya amewataka waumini kuhakikisha wanaweka utaratibu wa mpangilio wa ulaji kwa lengo la kujiepusha ma maradhi mbalimbali kwa kuwa hata Mungu kaisha weka utaratibu wa ulaji.
Pia amesema ili kuiweka afya katika kiwango kizuri ni vyema kufuata taratibu mzuri za ulaji ambao hauwezi kuwafanya mwili kuwa salama.
Katika hatua nyingine amewahimiza waumini kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao na wasiogope kufanya mazoezi ili kufanya mwili kuwa salama zaidi.
More Stories
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme