December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumishi wa Hospitali ya Amana watoa msaada kwa makundi maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Watumishi Wanawake Hospitali ya Mkoa Amana wametoa misaada Mbalimbali kwa watoto wenye Mahitaji maalum katika kituo cha Human Dreams Children’s Village kilichopo Tuangoma Wilayani Kigamboni.

Wakikabidhi msaada huo katika madhimisho ya siku ya wanawake Duniani Watumishi Wanawake wa Hospitali ya Mkoa Amana walisema wameweka utaratibu katika Hospitali hiyo kila mwaka katika madhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kutembelea watoto wa Makundi Maalum na kutoa misaada.

Watumishi Wanawake wameguswa na watoto wa utindio wa Ubongo mara nyingi wanapata Changamoto ya upumuaji hivyo vifaa hivyo vitawasaidia katika kutatua changamoto hiyo.

Wanawake wa Hospitali ya Mkoa Amana wametoa wito kwa wanawake wengine kusaidia vituo vya watoto wenye mahitaji Maalum.