Na Esther Macha, TimesmajiraOnline, Mbeya
WATUMISHI wa sekta ya afya nchini wametakiwa kuendelea kujifunza,kuboresha ujuzi , kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi na kuwa mfano katika uzalendo na utumishi bora kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo,Machi 1,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji wakati akizungumza na Madaktari Bingwa wa Masikio, Koo na Pua na Wataalamu wa Usikuvu nchini Tanzania walioweka kambi katika Mkoa wa Mbeya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu na huduma za uchunguzi wa awali wa masiko na usikivu.
Dkt . Mbwanji amesema kuwa huduma hizo zinatolewa bure bila malipo kwenye maadhimisho ya wiki ya Usikivu Duniani yanayofanyika kitaifa hospitalini hapo na kilele chake jumapili Machi 3,2024.
Aidha Dkt. Mbwanji amewapongeza wataalamu kwa juhudi zao za kutoa huduma za afya bora katika eneo la masikio, koo na pua, na kuwataka waendelee kuwa mfano wa uzalendo na utumishi bora kwa jamii.
“Naomba nitoe hamasa kwetu katika utendaji wetu kwenye taaluma yetu, ebu tuibuke na bunifu mbalimbali kwa kuwashirikisha wataalamu wenzetu wa Wahandisi vifaa tiba(Biomedical) na watu wa Tehama (ICT) kwa sababu tunaweza kuwa na mawazo na vitu vingine vikaitaji kutengenezwa hapa hapa na sisi guidance ikatoka kwetu, sisi tunaona na vijana wetu wana uwezo mkubwa sana.” – Dkt. Mbwanji
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalamu wa Masiko, Koo na Pua Dkt. Edwin Liyombo amesema lengo la uwepo wa siku ya usikivu duniani katika kuhamasisha wananchi, Wataalamu wa afya na watunga sera kuipa kipaumbele tatizo la usikivu kwa kuonyesha ukubwa wa tatizo watu wanaoweza kupata wasipopata huduma ya afya ya masikio na usikivu.
Pia ameshukuru uongozi na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma bora za afya, na kuahidi kuendelea kushirikiana na timu ya hospitali kwa lengo la kuboresha afya ya jamii.
Dkt. Mary Mathias Daktari Bingwa magonjwa ya Masikio, Koo na Pua kutoka hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ametoa wito kwa wananchi na Mkoa wa Mbeya na pembezoni kujitokeza kufanya uchukunguzi wa afya ya masikona usikivu bila malipo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ambapo kilele chake kitakua siku ya Jumapili tarehe 3 Machi 2024.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi