November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watumishi Housing waingia mkataba wa ujenzi wa nyumba-101-Dar

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

WATUMISHI housing Investment ( WHI) inatarajia kutekeleza MRADI wa nyumba 101 katika eneo la Mikocheni Regent Estate jijini Dar es salaam, ujenzi huo wa ghorofa 12 ambapo utaanza agosti mwaka huu.

Akizungumza jijini Mkurugenzi mtendaji wa shirika Hilo Fred Msemwa amesema ukamilifu wa ujenzi huo ni utekelezaji wa mpango wa makazi kwa watumishi wa umma ( Public servant Housing Scheme) unaotekelezwa na (WHI).

“WHI tayari imejenga nyumba 1003 katika mikoa 19 nchini Tanzania na nyumba 101 ambazo utoaji Saini na Mkandarasi Shadong Hi-speed Group umefanyika Leo julai 3 ni sehemu ya nyumba 218 zitakazojengwa katika mikoa ya Dodoma, Lindi , Mtwara, Singida , Pwani na Ruvima,” amesema Msemwa

Aidha Msemwa amesema kuwa ujenzi wa nyumba 101 utagharimu kiasi cha SHILINGI BILION 18.6 na ujenzi huo utafanyika kwa miezi 18 ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa utaratibu maalumu wa unafuu kwa watumishi wa umma, bei ya nyumba ya chumba kimoja yenye sebule ,chumba cha kulala ,choo, stoo ,jiko, balcony itaanzia SHILINGI million 99.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ,sebule , stoo balcony itaanzia SHILINGI milioni 234 ambapo bei za nyumba hizi zitakuwa zikilinganisha na nyumba zenye hadhi zilizipo maeneo ya Mikocheni.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa nyumba hizo gharama yake ni nafuu kwa kati ya asilimia 10 Hadi asilimia 40 ambapo uuzwaji wake tayari imeanza na wanatarajia kupata mwitiko mkubwa kutoka kwa walengwa, MRADI huu unalenga kuwapa watumishi wa umma fursa Bora za umiliki wa makazi yenye thamani.

Watumishi Housing Investment ni TAASISI ya umma chini ya ofisi ya Rais utumishi yenye jukumu la uendelezaji wa milki na usimamizi wa  uwekezaji kupitia uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja,WHI inasmamia mifuko miwili yaani mifuko wa nyumba pamoja na mfuko wa Faida Fund.

Kwa upande wake msaidizi wa Kampuni ya shadong Hi-speed Group Li Guangdong ameshukuru kwa kupata   zabuni hiyo ambapo wataitumia vema ili waweze kujitangaza kitaifa na kimataifa.

Mkurugenzi mtendaji wa Watumishi Housing Fred Msemwa (katikati)akitia Saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 101 na Kampuni ya kichina yenye thamani ya shilingi billion 18.6