Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kutuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Mizengo Pinda katika Manispaa ya Mpanda na kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja na kutishia kumuua kwa madai vinginevyo walipwe Milioni 50 ili wamwachie .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuhusika na tukio hili kuwa ni Joseph John(24) Yusuph Sadick (27) wakazi wa Mtaa wa Milupwa , Abrahamu Kassim(28) Mkazi wa Mtaa wa Misunkumilo Manispaa ya Mpanda na Samwel Nzobe (41) Mkazi wa Mtaa wa Kotasi Manispaa ya Mpanda .
Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa kufuatia msako mkali ulifanywa na jeshi la Polisi usiku na mchana ambapo wamefanikiwa kupata taarifa ya kutekwa kwa mtoto huyo mdogo wa kike .
Ngonyani amebainisha kuwa tukio hilo la kikatili la kumteka mtoto huyo lilitokea hapo June 13 majira ya saa nane mchana katika Manispaa ya Mpanda wakati mtoto huyo alipokuwa akitokea shuleni kwenye shule anayosoma ya Mizengo Pinda alikukuwa amekwenda kufanya usafi shuleni.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19