November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu 352 wafanyiwa uchunguzi wa moyo Dar

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

WATU 352 kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ambapo kati ya hao, 66 wamebainika kuwa na matatizo ya hayo.

Kaimu Mkurugenzi wa wa Taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete JKCI Hospitali ya Dar group Dkt Tulizo Shemu ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika kambi ya siku mbili ya matibabu ya uchunguzi ya ugonjwa wa moyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya moyo duniani

Amesema wagonjwa hao 66 ambao wamebainika kuwa na maradhi ya moyo wamepewa rufaa kutoka katika Hospital ya Dar group na kwenda katika Tiba kubwa zaidi katika Hospital ya Muhimbili JKCI .

“Wagonjwa hawa wamepelekwa katika Hospital ya Muhimbili JKCI ili waweze kushughulikiwa zaidi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya juu kwa lengo la kubaini matatizo makubwa walikuwa nayo pamoja na kufanya matibabu ya uhakika”amesema Dkt Shemu

Dkt Shemu aliongeza kuwa kufanya mazoezi ni mbinu kubwa ambayo mtu anaweza kuitumia kuweza kujikinga na maradhi ya moyo.

Amesema mbali na kufanya mazoezi pia mtu anashauriwa kupunguza unywaji wa pombe, kuacha kuvuta sigara, kupunguza ulaji wa vyakula kupindukia vyenye chumvi na sukari nyingi, matumizi ya mafuta mengi pamoja na ulaji wa waga

“Matibabu ya moyo ni gharama sana hivyo tumekuwa tukitoa ushauri Kwa watu kufanya mazoezi kwani asilimiaa 80 ya magonjwa hayo yanazuilika kwa mbinu hiyo” amesema Dkt Shemu

Na kuongeza kuwa
“Mazoezi ni kwa ajili ya afya ya binadamu ndio maana tunasema kabla ujaanza mazoezi lazima uijue afya yako pia mazoezi yanayoshauriwa kiafya ni mepesi na sio mazoezi magumu “alisisitiza

Kaimu Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa mazoezi mazuri yanayoshauriwa kwa afya ya binadamu ni mazoezi mepesi badala ya magumu kama vile kunyanyua vyuma vya kilo 100 … Bali ni yale ni mepesi yanayojumuisha kutembea, kukimbia.

Vilevile amesema mtu anapofanya mazoezi hayo mepesi anapaswa kuzingatia muda usiopugua dakika 15,20 hadi 30 na kuhakikisha yanakuwa ya kawaida na sio ya kushutukiza .

” Mazoezi mazuri kwa afya ni yale ambayo ni mepesi ambayo yanafanyika kila siku kwa dakika chache Ili kuufanya mwili wako kuwa vizuri.”amesema

Aidha amesema mazoezi hayo yanapaswa kuwa endelevu na mtu anapokuwa anafaya mazoezi hayo ni muhimu kuwa na maji ya kutosha kwani inashauriwa hivyo kitaaluma.

Hata hivyo amesema pindi mtu anapomaliza kufanya zoezi anashauriwa kuendelea kupasha mwili kwa kutembea tembea kidogo badala ya kulala na kuhakikisha anakula matunda au maji huku aliendelea kufanya mazoezi mepesi na badae kupata muda wa kupumzika.

Awali akizungumza mara baada ya kumaliza matembezi hayo Mkuu wa wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi aliiupongeza uongozi wa Taasisi ya Jakaya kikwete JKCI kwa kuchukua uamuzi wa kuadhimisha siku hii Kwa namna yake.

“Tunaipongeza JKCI kwa kuchukua maamuzi ya kuadhimisha siku hii Kwa namna yake pia tunatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha Kwa ajili ya sekta ya afya ambapo hivi Sasa kituo hiki Cha JKCI kinauwezo wa kutoa huduma si tu kwa watanzania hata kwa watu wa nchi Jirani”amesema Matinyi

Amesema hilo ndio lengo la kuamishia huduma hii katika kituo Cha Dar group kwa ajili ya kulenga watanzania wanaotoka mikoani pamoja na watu wanaotoka katika nchi jirani.

Baadhi ya watu waliudhulia katika kambi hiyo ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo