January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu 108,371 wapatiwa chanjo ya UVIKO-19

Judith Ferdinand, Mwanza, TimesMajira Online

Imeelezwa kuwa hadi kufikia Desemba 6,mwaka huu jumla ya watu 108,371,mkoani Mwanza wamepatiwa chanjo ya UVIKO-19 kwa dozi ya kwanza.

Hayo yalielezwa na Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja,wakati akiwasilisha taarifa ya chanjo na uchanjaji kwa Mkoa wa Mwanza,katika
kikao cha huduma za afya na vifo vya wazazi na watoto wachanga,kilichofanyika mkoani hapa.

Kiteleja amesema,utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ulianza Agosti 3,2021 katika Mkoa mzima wa Mwanza huku walengwa ni watu wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Ambapo dozi ya kwanza watu idadi ya watu 108,371 huku idadi ya 9,735 dozi ya pili wamepata chanjo ya UVIKO-19 kwa Mkoa mzima wa Mwanza.

“Awamu ya kwanza tulianza kutoa chanjo aina ya Janssen ambayo ilimalizika Oktoba 18,2021,awamu ya pili tulianza kutoa chanjo aina ya Sinopharm kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2021,chanjo hii hutolewa dozi mbili kwa utofauti wa wiki nne,”amesema Kiteleja.

Pia amesema hakuna mteja aliyepata maudhi makubwa baada ya kupatiwa chanjo hiyo tangu kuanza kwa zoezi hilo,hivyo uchanjaji unaendelea hadi asilimia 60 ya watu wote katika Mkoa huo wapatiwe chanjo ya UVIKO-19.

Huku akiongeza kuwa wakati wowote watapokea chanjo aina ya Pfizer ambayo itatolewa kwa dozi mbili kwa utofauti wa wiki nne pia

Sanjari na hayo amesema, aina mpya ya kirusi kinachosababisha ugonjwa wa UVIKO-19,kimetokana na mabadiliko (mutations) ya kirusi cha UVIKO-19.

Ambapo utafiti na ufuatiliaji unaendelea katika nchi kadhaa zilizoripoti uwepo wa virusi hivi,kujikinga na ugonjwa huu, tahadhali zote za UVIKO-19 ziendelee kuchukuliwa.

Aidha amesema kila mkoa ujipange kutoa chanjo kwa wateja wasiopungua 3,000 kwa siku huku kila halmashauri ichanje watu si chini ya 600 kwa siku na vituo vichanje si chini ya watu 20 kwa siku.

“Utoaji wa chanjo kila siku ulenge kufikisha chanjo karibu kabisa na wananchi,huduma tembezi zifanyike katika maeneo ya mikusanyiko hususani sokoni na sehemu za ibada pamoja na maeneo mengine,”.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakati akifungua kikao hicho,amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na UVIKO-19 kwani baadhi ya nchi duniani wapo kwenye mlipuko wa wimbi la nne la maambukizi hayo .

Mhandisi Robert amesema, tahadhari zote zichukuliwe ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima,kunawa mikono,kutumia kitakasa mikono ,kuchanja na kuvaa barakoa.

Amesema maeneo yote ya serikali yanayotoa huduma zoezi la barakoa lirudi kwenye milango ya kuingilia watu wavae kwa sababu kirusi hicho namba nne kipo njiani,wanahitaji wananchi wapate huduma wakiwa salama .

” Tunahitaji kuhudumia wananchi tukiwa na afya njema kwa sababu tunamiradi mbalimbali ambayo bado inaendelea kutekelezwa tahadhari lazima zichukuliwe ili tuwe na afya njema,”amesema Mhandisi Robert.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria kikao cha
kikao cha huduma za afya na vifo vya wazazi na watoto wachanga,kilichofanyika mkoani hapa.

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja,wa pili kutoka kulia akufuatilia jambo wakati
kikao cha huduma za afya na vifo vya wazazi na watoto wachanga,kilichofanyika mkoani hapa.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria kikao cha
kikao cha huduma za afya na vifo vya wazazi na watoto wachanga,kilichofanyika mkoani hapa. Picha na Judith Ferdinand