December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watoto 80,486 kufikiwa na kamapeni ya Chanjo ya Polio Wilayani Kalambo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikina na wizara ya afya imepanga kuendesha kamapeni ya polio kwa mikoa minne inayopakana na nchi za Zambia ikiwemo mkoa wa Rukwa,katavi , Songwe na Mbeya ili kuwakinga watoto chini ya miaka 5 dhidi ya ugonjwa huo.

Hayo yamebainishwa na kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Dr.Emmanuel Kisyombe kupitia kikao cha kamati ya afya ya msingi (PHC) kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Ambapo amesema kampeni hiyo inarajiwa kuanza Julai 27/2023 na kuhitimishwa Julai 30/2023.

‘’Chanjo ambayo itatumika katika kampeni hii ni chanjo ya polio ya sindano (IPV) ambayo ina mpa kinga mtoto dhidi ya Polio virus type 2’’na kwamba zaidi ya watoto 80,486 wanatarajiwa kufikiwa kupitia kampeni hiyo’’ alisema Dr Kisyombe.

Mapema akizungumza kupitia kikao hicho mwenyekiti wa kamati ya afya ya msingi ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba aliwataka wataalamu wa afya wilayani humo kuendelea kushirikiana na wadau wakiwemo viongozi wa dini katika kudhibiti ugonjwa kwa kutoa elimu kwenye maeneo ya mikusanyiko, makanisani na misikitini ili kuwezesha watoto wengi zaidi kupata chanjo hiyo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Polio ni ugonjwa unao sababisha ulemavu na tishio la maisha unatokana na maambuzi ya virus vya polio na kwamba dalili zake ni pamoja na maumivu ya kichwa, mwili kuchoka, kuchefuchefu na maumivu ya tumbo.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Razaro Komba akizindua zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio kwa Watoto walio chini ya miaka mitatu