Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Licha ya sekta ya habari za mtandaoni kukua imeelezwa kuwa imekuwa na changamoto ya kile kinachoandikwa kwenye kichwa cha habari hakiaendani na maudhui yaliomo katika habari husika.
Hivyo waandishi wa habari wa vyombo vya habari za mtandaoni wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na maadili kwa kuhakikisha kichwa cha habari kinaendana na maudhui ya habari husika.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo, wakati akifungua kikao kazi na watoa huduma wa maudhui mtandaoni Kanda ya Ziwa uliofanyika jijini Mwanza kilichoandaliwa na TCRA.
Mhandisi Mihayo, ameeleza kuwa unakuta baadhi ya vyombo vya habari vya mtandaoni vimeandika kichwa cha habari kuwa “imeisha hiyo” lakini ukifungua link yake kuanzia mwanzo hadi mwisho unakutana na sauti ya mtangazaji ikusema neno”Subscribe”bonyeza kengele’ kwa habari zaidi.
“Kwa wataalamu wenye leseni kutoka TCRA sitegemei muwe na kitu kama hicho na mfanye kazi kwa kuzingatia maadili pia siyo mtumishi wa taasisi fulani akiwa amefanya jambo au kosa huko kwenye habari badala ya kumandika muhusika unaunganisha na taasisi anayifanyia kazi,”ameeleza Mhandisi Mihayo.
Mwanasheria wa TCRA Joseph Kavishe,ameeleza amewataka waandishi wa habari hao kuwa vichwa vya habari vya kuvutia ziendane na habari yenyewe na yale wanayoandika yazingatie kujenga kizazi chao.
Kavishe ameeleza kuwa jukumu la mamlaka hiyo ni kuhakikisha watoa huduma wanazingatia maadili,kanuni na sheria huku wajibu wake ni kutoa elimu.
“Tuzingatie kanuni ya utoaji maudhui mtandaoni,ulinzi na usalama wa taifa,tunawajibu wa kulinda nchi,kizazi chetu na maudhui yatakayowekwa leo hadi wajukuu wako watayakuta hivyo tunawajibu wa kulinda kizazi chetu,tunapopiga picha za ajali tuhifadhi utu wa mtu ata kama amekufa,” ameeleza Kavishe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) Edwin Soko, ameeleza kuwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wanahitaji sana mafunzo ili kuwajengea uwezo katika masuala la usalama wa waandishi wa habari hususani katika mitandao.
Hivyo amewataka waandishi hao kuwa makini na mambo ambayo ya yanayoashiria vitisho vya kimtandao ikiwemo kubonyeza viunganishi ‘links’ zinazoshawishi kwamba umeshinda zawadi (phishing) pamoja na kuhakikisha wanaweza nywila ambayo utakuwa ngumu katika vifaa vyao.
Naye Mwenyekiti Mstaafu wa MPC Deus Bugaywa, ameeleza kuwa waandishi wa habari za mtandaoni washindane katika kurusha maudhui ya uhakika kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
“Msingi mkubwa wa waandishi wa habari ni maadili,tunawajibu wa kuzingatia na kulinda jamii yetu,”ameeleza Deus
Kikao hicho chenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari wanaorusha maudhui mitandaoni Kanda ya Ziwa ili waweze kuwa na uelewa juu ya kanuni na maadili ya uandishi habari ili kuepuka makosa ya mara kwa mara yanayojitokeza katika uwasilishaji wa maudhui mtandaoni.
More Stories
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA
Mwanafunzi apoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba
Mwanafunzi adaiwa kuuwawa na rafiki wa baba yake